Powered By Blogger

Sunday, July 1, 2018

MAFUNDISHO YA NDOA SEHEMU YA KWANZA

MAFUNDISHO YA NDOA

UTANGULIZI:
    Hadhi na  heshima ya ndoa inaendelea kushuka katika miaka hii ya Sayansi na Teknologia.       Maendeleo makubwa ya Sayansi yanaonekana duniani na hivyo ingetakiwa pia maisha ya ndoa yastawishwe zaidi lakini kinyume chake ndiyo mporomoko unaongezeka. Migogoro, Ndoa za mitara kutengana na kuachana ndiyo mambo yanayosikika kila pande ya dunia. Watoto wa mtaani wanaongezeka, magonjwa ya kuambukiza yanayosababishwa na zinaa hata ndani ya ndoa yanasikika.
            Swali; Hali hii itapata uponyaji wapi?
     Kupata uponyaji wa jambo hili, ni kuliponya Kanisa linalohangaika, kwa njia ya Imani thabiti, mafunzo na mafundisho ya familia, kudumisha utamaduni na mila njema, kuendeleza maadili mema kuanzia kwenye   mizizi (root)
     Ndoa ni kuungo bora cha muhimu katika msingi wa mwanadamu kinachoashiria Umoja, Upendo, Amani na Utulivu.
     Karibuni basi tutafakari pamoja kuhusu Ndoa, uuzuri wake, changamoto zake na nini cha kufanya katika kuboresha ndoa zetu ili kanisa liweze kustawi zaidi.




MAANA HALISI YA NDOA:
     Maandiko matakatifu huanza na uumbaji wa mwanaume na mwanamke kwa sura na mfano wa Mungu na humalizika na maono ya “arusi za mwanakondoo” (Uf. 19:9). Hivyo tunaweza kusema ndoa ni muunganiko wa mwanamke na mwanaume kwa hiari na kufuata utaratibu wa Kanisa. Wito wa ndoa umeandikwa katika maumbile yenyewe ya mwanaume na mwanamke kama walivyo toka mikononi mwa muumbaji.
      Mwanaume na mwanamke waliumbwa mmoja kwa ajili ya mwingine
“Si vema mtu huu awe peke yake (Mw. 2:18) mwanamke ni nyama na ubavu wa mwanaume. Asili yao ni moja. Kwa sababu hiyo mwanaume atamwacha Baba yake na Mama yake naye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja (Mw. 2:24). Hata wamekuwa si mwili tena bali mwili mmoja” (Mt. 19:6).
      Vurugu, ghasia zote za ndoa zimetawaliwa na dhambi ya mwanzo iliyovunja uhusiano wa asili wa Mume na Mke kama tokeo la kwanza. Mahusiano hayo yameharibiwa na kulaumiana kati yao (Mw. 3:12) mvuto kati yao, kipaji chao toka kwa Muumba chabadilika kuwa mahusiano ya uonevu na tamaa mbaya, wito mzuri wa mume na mke wa kuzaa na kuongezeka na wa kuitisha nchi umegandamizwa na uchungu wa kuzaa na taabu ya kufanya kazi (Mw. 1:28` 3:16-19).

Line Callout 1: 1 



mama wanapata msisimko palepale na kushuka taratibu na kurudi ni
ngumu zaidi kuliko  wanaume hivyo katika mahusiano ya ndoa inapaswa mwanamke aandaliwe vizuri tena  kwa muda mrefu.
        Kwa kadiri utakavyofanya mapenzi na mke wako ndivyo unadhihirisha upendo wa kweli kadiri ya muda unavyoenda na kadiri utakavyoendelea kumsoma mkeo.
        Muhimu ni kuwa mkweli na muwazi kwa (Be honest), katika mahusiano ya kindoa usijiangalie wewe peke yako bali umuone na mwenzi wako. Kila mmoja anahitaji.
       Kuna msemo usemao “Wakina mama wengi hawana hamu ya kufanya  mapenzi (frigiolity),! Inawezekana  lakini kiukweli ni kiasi kidogo sana. Mwanaume unaweza kumfanya mkeo awe hivyo. Ubinafsi na kutokujua (Ignorance) kwa mwanaume kunaweza kumkosesha furaha mkeo maisha yake yote. Kuepukana na hilo mambo mawili yafanyike:
1.      Hakikisha kuna  upendo wa dhati (AGAPE) hata kitandani; ‘Agape ni upendo unaotafuta furaha kwa kutoa na  kupokea. Kuondoa aina yoyote ya ubinafsi katika ndoa.
2.      Kujua ni kitu gani kinampa mke wako furaha ya kimapenzi na ufanye hivyo. Unaweza kumfikisha mke wako kileleni…,?? Mjue mkeo vizuri.

     Katika mahusiano ya kindoa kwa mwanamke kuna njia 5 za kufuata ili mkeo afurahie uwepo wako kwako: Kimapenzi..!
1)      Maandalizi.
2)      Mawasiliano
·         Clitons & Velva (masikio, pua, mapaja, macho, mdomo, shingo, maziwa, mifereji..)

3)      Kuingia katika  kitendo hicho (mapenzi) Sexual  Intercourse.
·         Usiharakishe
·         Mpaka yeye mwenyewe aamue
·         Mpaka ute utoke

4)      Kufikia kilele (Orgasn).
·         Mwanaume once
·         Mwanamke-mara 3 hadi 4

5)      Baada ya kitendo hicho (real life)-usipumzike mara shukuru, mwonyeshe kwamba umeridhika.
Tormular;  Mwanaume anapenda ili ‘kupata mapenzi’.

Mwanamke anatoa mapenzi ili ‘kupendwa au kupata upendo’

No comments: