Powered By Blogger

Wednesday, January 30, 2019

KIONGOZI NI NANI


KIONGOZI NI NANI
Sehemu  Ya  Kwanza
  Kiongozi:  Ni mtu anayechaguliwa au kuteuliwa na watu ili utekeleza yale yanayotakiwa kutekelezwa.  Au Kiongozi: Ni mtu anayechaguliwa na watu ili kuwa mwaakilishi wao katika Taasisi au Jumuiya ya watu flani.
            Watu wanaweza kuwa viongozi kutokana na sifa au karama aliyojaliwa na Mungu. Kiongozi naweza akawa mtu aliyesomea pia kuna baadhi ya watu wao huzaliwa wakiwa na  karama hiyo ya uongozi, watu hawa wanaweza wakawa viongozi wazuri sana pengine kupita hata wale waliosomea.
            Katika ulimwengu watu kuna aina mbili za viongozi;-
1.         Viongozi wa kuchaguliwa
2.        Viongozi wa kuteuliwa/kurithi

****************
MAJUKUMU  YA  KIONGOZI;-
         i.            Kutekeleza majukumu aliyopewa na watu
       ii.            Kuwaunganisha watu
     iii.            Kusimamia raslimali za watu
      iv.            Kusimamia na kulinda “ukweli”  katika kuleta maendeleo ya watu
Kiongozi akitimiza majukumu hayo atakuwa ni kiongozi mzuri na mwenye kupendwa na watu kwa sababu ya  utumishi wake mzuri kwa watu. Watu wanaweza kutamani na kuonja maisha ya furaha kupitia yeye, na ndivyo ilivyo kwa kiongozi mzuri anayejali na kutekeleza majukumu yake.
UONGOZI  MBAYA;-
             Katika uongozi kuna baadhi ya watu wao hutumia Mamla hayo ya uongozi kufanya ndivyo sivyo kwa sababu ya manufaa yao binafsi. Jambo hili huathili sana watu wanyonge wanaotegemea viongozi wao kufaya kadri ya matakwa na misingi ile uliyompelekea yeye kuchaguliwa au kuteuliwa na watu.  Kiongozi anaweza akawa kikwazo kwa watu kwa sababu ya kutumia nguvu na mamlaka aliyopewa kunyanyasa watu na kuhujumu mali na haki ya binadamu.

            Asilimia kubwa ya watu wanaotarajia kuteuliwa au kuchaguliwa huwa ni wazuri wa kushawishi na huwa wanamvuto flani kabla hawajawa viongozi, hawa hufanya hivyo kwa sababu bado hawajapata uongozi, na huwa ni watu wa watu sana.
           Uongozi vile vile unaweza kumtia mtu ‘ujinga’ au ‘ukatili’ kwa sababu ya mitazamo binafsi. Uongozi  unawafanya viongozi wa Serikali pia Dini, kutumia uongozi huo waliopewa kunyanyasa watu.  Wao hujiona ni bora sana kupita watu wengine, wao hujiona si wakosefu, wao hujiona wapo sawa katika kile wanachokifanya, wao huyaona makosa ya watu wengine kuliko yao, wao hulimbikiza makosa yao kwa vijakazi wao waonekane wazuri, wao huwaona ni watumwa na watu wasiojielewa watumishi wengine. Hizi ni baadhi ya sifa za viongozi wanaotumia mamlaka yao vibaya.

********************************
Inaendelea……………………………..











Mayumba Publisher
Msalala-Kahama, Contact. +2257-6925-3139
Author; John  Christopher

Email.  Johnchristopher220@gmail.com,  Contact; +2257-5509-2885


ROZARI  YA  HURUMA  YA  MUNGU

HISTORIA  YA  TOKEO  LA  HURUMA  DUNIANI
       Sista Faustina alizaliwa tarehe 25 August 1905 katika kijiji cha Glogowieko nchini Poland, na jina lake la ubatizo lilikuwa Helena.
        Akiwa na umri wa Miaka 20, Bwana alimwongoza kuingia katika utawa wa shirika la Mama wa Huruma ambako (kama kawaida) alibadilisha jina na kuitwa Sista Maria Faustina, akaweka nadhiri za kwanza mwaka 1928.

MATUKIO
         Bwana Yesu alianza kumtokea Sista Faustina mfululizo tangu mwaka 1930 hadi 1938. Alimtokea ili kumwandaa kwa ujumbe mkubwa wa maisha wa kuiangazia dunia nzima Ibada ya Huruma ya Mungu, ambayo ilikuwa na madhumuni yafuatayo;
  1. Kuandaa ujio wa Pili wa Bwana wetu Yesu Kristo aliye Mfalme wa Huruma.
  2. Kuokoa roho zilizoko Toharani.
  3. Kuwaongoa wakosefu ambao wameshapoteza neema ya kujiombea.
  4. Kuitangaza Huruma ya Mungu.

        Tarehe 22 Februari 1931 alipokuwa na umri wa miaka 26, Sista Faustina alitokewa kwa mara ya kwanza na Bwana Yesu na kumchagua kuwa mjumbe wa Ibada ya Huruma ya Mungu. Sista Faustina anatueleza:

"Jioni, ndani ya chumba changu, huku nikiwa nimepiga magoti kwa woga na furaha, nilimuona Bwana Yesu akiwa amevaa vazi refu jeupe. Aliinua mkono juu kwa kubariki, na mkono mwingine ulishika nguo yake kifuani. Kutoka ndani ya nguo kifuani kulitokea miale ya aina mbili ya

"Mchoro halisi wa Huruma Kuu, uliochorwa
 chini ya usimamizi wa Sista Faustina"

 mwanga inayong'ara. Miale ya upande wa kulia ilikuwa myekundu na miale ya upande wa kushoto ilikua myeupe"
       Sista Faustina hakujua maana ya aina hizo mbili za miale ya mwanga aliyoiona, na siku moja alimuuliza Bwana Yesu maana yake. Bwana Yesu kwa utulivu mkubwa alimwambia, "Miale miwili hiyo ya mwanga inayotoka ndani ya moyo wangu ni alama ya Damu na Maji yaliyomwagika kutoka katika Moyo wangu wenye Huruma, siku ile nilipojitoa sadaka Kalvarini. 
Miale Myeupe ni alama ya Maji yanayoosha roho na miale Myekundu ni alama ya Damu inayoleta uzima wa Roho za watu. Miale hii inalinda Roho kabla ya adhabu ya Baba yangu: Kwa anayeishi katika ulinzi wake (Miale hiyo), mkono wa Hasira ya Mungu hautamfikia kamwe’’.
      Kisha Bwana Yesu alimfundisha Sista Faustina sala hii: "Ee Damu na Maji vinavyotoka katika Moyo Mtakatifu wa Yesu, kama chanzo cha Huruma yake, ninakutumaini"
      Bwana Yesu huku akimwonyesha Moyo wake Mtakatifu alimwambia Sista Faustina "Chora picha kama unavyoona, na  uandike YESU NINAKUTUMAINIA. Mimi ni Mfalme wa Huruma.
      “Ninatamani picha hii iwekwe na kuheshimiwa kwanza Kanisani kwako na baadaye Ulimwenguni kote. Naahidi ushindi kwake na maadui zake walio Duniani na hasa saa ya kufa kwake. Mimi mwenyewe nitamlinda. Kwa njia ya picha hii nitatoa neema nyingi kwa watu watakaoitunza vizuri, hata kwa wale watakaoitazama"





1.     Ishara ya Msalaba
2.     Baba Yetu
3.     Salamu  Maria
4.     Kanuni  ya  Imani

    Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi, Muumba mbingu na Dunia na kwa Yesu Kristo, Mwanaye wa pekee Bwana wetu, aliyetungwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo  Pilato, akasulibiwa, akafa, akazikwa akashukia kuzimu siku ya tatu akafufuka kadiri ya maandiko, akapaa mbinguni ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu, Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa Takatifu Katoliki, Ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi , Ufufuko wa Miili na Uzima wa Milele. Amina

5.     Baba wa Milele, ninakutolea Mwili na Damu, Roho na Umungu wa Mwanao Mpenzi sana, Bwana wetu Yesu Kristo, Kwa malipizi ya dhambi zetu na za Dunia nzima.
6.     K.  Kwa ajili ya mateso makali ya Bwana     
               wetu Yesu Kristo.
        W.  Utuhurumie  sisi na Dunia nzima

7.     MWISHO
         K.     Ewe Damu na Maji aliyemwagika kutoka Moyoni
  mwa  Yesu kama Chemuchemu ya Huruma kwetu.
         W.   Tunakutumainia
         K .    Mungu Mtakatifu,
                  Mtakatifu Mwenye Enzi,
                  Mtakatifu unayeishi milele  x 3
         W.   Utuhurumie  sisi na Dunia nzima


LITANIA YA HURUMA YA MUNGU

Bwana utuhurumie – - -                               Bwana utuhurumie
Kristu utuhurumie – - -                                Kristu utuhurumie
Bwana utuhurumie – - -                               Bwana utuhurumie
Kristu utusikie – - -                                         Kristu utusikilize
Baba wa mbinguni Mungu – - -                                           utuhurumie
Mwana Mkombozi wa dunia Mungu - - utuhurumie
Roho Mtakatifu Mungu - - -                                                  utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu mmoja                                                          utuhurumie.
Huruma ya Mungu iliyo sifa kuu ya Muumba wetu - - -
Tunakutumaina
Huruma ya Mungu iliyo kilele cha ukamilifu wa Mwokozi wetu
Tunakutumaina
Huruma ya Mungu iliyo upendo usiopimika wa Roho Mtakasa
Tunakutumaina
Huruma ya Mungu fumbo lisilofahamika la Utatu Mtakatifu
Tunakutumaina
Huruma ya Mungu iliyo ishara ya uwezo mkuu wa Mungu Mwenyezi                                                               Tunakutumainia
Huruma ya Mungu iliyofumbuliwa katika kuziumba Roho za Malaika wa mbinguni                                                  Tunakutumainia
Huruma ya Mungu iliyotuumba na kutuamuru tuwepo bila kutokana na chochote                                                    Tunakutumainia
Huruma ya Mungu inayotujalia maisha ya kutokufa
Tunakutumaina
Huruma ya Mungu inayotukinga na adhabu tunazostahili
Tunakutumaina
Huruma ya Mungu inayotuinua tutoke katika taabu, unyonge na maumivu ya dhambi zetu                      Tunakutumainia
Huruma ya Mungu inayotufanya wenye haki katika Neno aliyejifanya Mtu                                       Tunakutumainia
Huruma ya Mungu iliyotupatia Bikira Maria Mtukufu awe kwetu Mama wa Huruma                   Tunakutumainia
Huruma ya Mungu iliyoonyeshwa katika kuanzishwa Kanisa Katoliki                                                  Tunakutumainia
Huruma ya Mungu inayopatikana katika mafumbo ya Sakramenti Takatifu                                     Tunakutumainia
Huruma ya Mungu inayotolewa kwa wanadamu wote kwa njia ya Sakramenti ya Ubatizo na Kitubio Tunakutumainia
Huruma ya Mungu inayotolewa katika Sakramenti ya Ekaristi na Upadrisho                                                   Tunakutumainia
Huruma ya Mungu inayoonyeshwa kwetu pale inapotuita na kutuingiza katika kuwatakatifuza wenye hakiTunakutumainia
Huruma ya Mungu inayotimilika katika ukamilifu wa watu watakatifu                                                              Tunakutumainia
Huruma ya Mungu chemchemi ya afya kwa wagonjwa na wote wanaoteseka                                                 Tunakutumainia
Huruma ya Mungu iliyo faraja ya wote wenye uchungu moyoni
Tunakutumaina
Huruma ya Mungu iliyo tumaini la roho zinazosumbuliwa na mkato wa tama                                                Tunakutumainia
Huruma ya Mungu iliyo mwenzi wa daima na popote wa watu wote                                                                   Tunakutumainia
Huruma ya Mungu inayowahi kutuletea neema zake
Tunakutumaina
Huruma ya Mungu iliyo amani yao wanaokufa
Tunakutumaina
Huruma ya Mungu iliyo burudisho na faraja yao marehemu wa toharani                                                           Tunakutumainia
Huruma ya Mungu iliyo furaha ya mbinguni kwa watakatifu wote                                                                        Tunakutumainia
Huruma ya Mungu iliyo taji la watakatifu wote
Tunakutumaina
Huruma ya Mungu chemchemi ya miujiza isiyokauka
Tunakutumaina
Huruma ya Mungu inayofurika kutoka katika majeraha ya Kristu                                                                                          Tunakutumaina
Huruma ya Mungu inayobubujika kutoka ndani ya Moyo Mtakatifu wa Yesu                                                   Tunakutumaina

Mwanakondoo wa Mungu uliyetuonyesha huruma yako kuu

katika kuikomboa dunia kwa msalaba wako mtakatifu, -
utusamehe ee Bwana

Mwanakondoo wa Mungu unayejitolea kwetu kwa mapendo na
huruma katika kila adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu,-
utusikilize ee Bwana

Mwanakondoo wa Mungu anayeondoa dhambi za dunia kwa njia ya huruma yako isiyo na mwisho,-                 utuhurumie.

K.                           Bwana utuhurumie –
W.                          Bwana utuhurumie.
K.                            Kristo utuhurumie, -
W.                          Kristo  utuhurumie
K.                            Huruma anana za Bwana zi juu ya kazi zake
zote –
W.                          Huruma za Bwana nitaziimba milele.


TUOMBE:
       Ee Mungu uliye na huruma isiyo na mwisho, na hazina za wema na upendo wako hazina mipaka. Tunakusihi ututazame sisi watu wako huku duniani na kutuongezea huruma yako tena na tena, ili itusaidie tusije tukakata tamaa hata mara moja, haidhuru tukumbane na majaribu makubwa kiasi gani, bali tuweze daima kuzielekea na kuzishika amri zako, kwa matumaini na kutimiza mapenzi yako matakatifu, ambayo ndiyo huruma yenyewe. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristu Mwanao, Mfalme wa Amani na Huruma, aishiye na kutawala nawe, na Roho Mtakatifu, kwa pamoja mkituonyesha huruma, daima na milele. Amina.




 

ROZARI  TAKATIFU YA BIKIRA  MARIA
HISTORI  FUPI  YA ROZAR  YA BIKIRA  MARIA
        Neno Rozari limetokana na neno la Kilatini  "Rosarium" lenye maana ya Taji la Mawaridi. Neno “WARIDI” katika maana halisi na sahihi ni ni moja kati ya Ua lenye muonekano Mzuri na lenye kuvutia sana kwa maana fupi Waridi ni  “Alama ya Ushindi” na sisi Mama Maria anatuhimiza tumweze kumpa “Waridi” kila tusalipo Rozari kwa kuwa katika Rozari ndiko Upendo wake kwetu ulimo. Mama yetu Bikira Maria aliwafahamisha baadhi ya watu aliowatokea kuwa kila mara mtu anaposali sala ya "Salamu Maria" anampa mama Maria waridi na hivyo kila anayesali rozari nzima humkabidhi mama Maria taji la mawaridi. Rozari imegawanyika katika matendo yafuatayo: Matendo ya FURAHA, UCHUNGU na UTUKUFU.   Na mnamo October 16, 2002 Baba Mtakatifu marehemu John Paul II aliongeza matendo mengine ambayo yaliitwa matendo ya  MWANGA. Rozari Takatifu hujulikana kama sala kamili kwa sababu ndani yake hupatikana Historia kamili ya ukombozi wetu sisi wanadamu. Katika Rozari tunatafakari matendo ya Furaha, Uchungu na Utukufu ambayo yanaelezea historia nzima ya maisha ya Bwana wetu YESU KRISTO na ukombozi uliopatikana katika yeye kwetu sisi wanadamu kupitia Msalaba.

      Katika sala ya Salamu Maria tunamkaribisha Mama Maria atuombee sisi wanadamu kwa mwanawe Bwana wetu YESU KRISTO hivyo kufanya sala zetu kuwa na nguvu zaidi mbele zake MUNGU.
Yesu hawezi kukataa maombi ya Mama yake na hivyo ni wajibu wetu  kufanya bidii katika kusali Rozari Takatifu ya Mama yetu Bikira Maria.
        Dhumuni kuu la kusali rozari ni kwa ajili ya kuwaombea wakosefu waongoke na kumrudia MUNGU katika KRISTO YESU mwanawe wa pekee aliyetukomboa dhidi ya yule muovu kwa mateso, kifo na ufufuko wake. Kila mara mtu au watu wanapopiga magoti na kusali rozari mama Bikira Maria huja haraka na kukaa pembeni yake/yao wanaosali na kusali nao,

NAMNA  YA  KUSALI  ROZARI  YA  BIKIRA  MARIA












 










Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina
(Tunasali Rozari Takatifu kwa Nia ya /………………../)

1.       KANUNI  YA  IMANI (kwenye Msalaba)

        Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi, Muumba mbingu na Dunia na kwa Yesu Kristo, Mwanaye wa pekee Bwana wetu, aliyetungwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo  Pilato, akasulibiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu siku ya tatu akafufuka kadiri ya maandiko,akapaa mbinguni ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu, Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa Takatifu Katoliki, Ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi , Ufufuko wa Miili na Uzima wa Milele. Amina
 

  2.          Baba Yetu  (Punje  Kubwa)
3.          Salamu  Maria x 3 (Punje  ndogo)

4.          Atukuzwe  Baba……. (Kwenye punje Kubwa)
                K.  Tuwasifu  Milele
              W. Yesu  Maria na Yoseph

              K.  Ee  Yesu  Mwema
              W. Utusamehe  dhambi zetu utukunge na moto wa Milele
      ongoza Roho zote Mbinguni, hasa za wale wanaohitaji  
      huruma yako
                Taja fumbo kisha (Baba Yetu)
  5.          Salamu  Maria x 10
  6.          Atukuzwe  Baba……. (Kwenye punje Kubwa)
              K.  Tuwasifu  Milele
              W. Yesu  Maria na Yoseph

              K.  Ee  Yesu  Mwema
              W. Utusamehe  dhambi zetu utukunge na moto wa Milele
       ongoza Roho zote Mbinguni, hasa za wale wanaohitaji 
       huruma yako

MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)

Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu  atujalie unyenyekevu.

Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la tano
; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.

MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)

Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la pili;
Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la tatu;
Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la nne
; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano
; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)

Tendo la kwanza;      Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie    kugeuka watakatifu.
Tendo la pili;
Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwendambinguni.
Tendo la tatu;
Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne;
Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
Tendo la tano
; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)
TENDO LA KWANZA; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
TENDO LA PILI;
Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
TENDO LA TATU;
Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
TENDO LA NNE;
Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
TENDO LA TANO;
Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
SALAMU  MALKIA
Mama mwenye huruma, uzima, tulizo na matumaini yetu, salamu, tuankusihi ugenini hapa sisi wana wa Eva. Tunakulilia, tunalalamika na kuhuzunika bondeni huku kwenye machozi.  Haya basi mwombezi wetuutuangalie kwa macho yako yenye huruma. Mwisho wa ugeni huu, utuonyeshe Yesu mzao wa tumbo lako.  Ee mpole, Ee mwema, Ee  mpendelevu,  Bikira  Maria.

K.            Utuombee mzazi Mtakatifu wa Mungu
W.          Utujalie ahadi ya Kristo

Tuombe:  Ee  Mungu, makimbilio na nguvu yetu, uwaangalie kwa wema watu wanao kulilia; na kwa maombezi ya Bikira Maria Mtukufu asiye na kosa Mzazi wa Mungu, na ya Mtakatifu Yosefu, mchumba wake, na ya Watakatifu wote: usikilize kwa huruma na wema sala tunazokutolea kwa wongofu wa wakosefu na kwa

KUMBUKA
    Kumbuka Ee Bikira mpole sana, haijasikilika kamwe kwamba ulimwacha mtu aliyekimbilia ulinzi wako, aliyeomba msaada na maombezi yako.
     Kwa matumaini hayo, nakukimbilia, Ee Mama, mkuu wa mabikira.  Ninakuja kwako, nasimama mbele yako, nikilalamika mimi mkosefu , Ewe Mama wa Neno wa Mungu. Naomba usikatae  maneno yangu, bali uyasikilize. Amina
(Tunakimbilia Ulinzi wako……………………………….)
 

LITANIA YA BIKIRA MARIA

Bwana utuhurumie                                Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie                                 Kristo utuhurumie
Bwana utuhurumie                                Bwana utuhurumie
Kristo utusikie                                          Kristo utusikilize

Baba wa Mbinguni  Mungu,……                         Utuhurumie
Mwana Mkombozi wa dunia Mungu………   Utuhurumie
Roho Mtakatifu Mungu……..                               Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja ……..              Utuhurumie
Maria Mtakatifu ……….                                          Utuombee
Mzazi Mtakatifu wa Mungu ……..                     Utuombee
Bikira Mtakatifu Mkuu wa Mabikira ……..    Utuombee
Mama wa Kristo ………                                          Utuombee
Mama wa Neema ya Mungu …………..             Utuombee
Mama Mtakatifu sana ………                               Utuombee
Mama mwenye usafi wa Moyo ………..          Utuombee
Mama usiye na doa ………..                                  Utuombee
Mama usiye na dhambi……                                 Utuombee
Mama mpendelevu ……….                                   Utuombee
Mama mstajabivu ……….                                      Utuombee
Mama wa shauri jema                                          Utuombee
Mama wa Muumba ……….                                   Utuombee
Mama wa Mkombozi …………..                          Utuombee
Bikira mwenye utaratibu …………..                 Utuombee
Bikira mwenye heshima …………..                    Utuombee
Bikira mwenye sifa …………..                              Utuombee
Bikira mwenye enzi …………..                             Utuombee
Bikra mweye huruma …………..                         Utuombee
Bikra amini…………..                                               Utuombee
Kioo cha haki …………..                                          Utuombee
Kikao cha hekima …………..                                                 Utuombee
Sababu ya furaha yetu …………..                        Utuombee
Chombo cha neema …………..                             Utuombee
Chombo cha heshimiwa …………..                    Utuombee
Chombo bora cha Ibada …………..                     Utuombee
Waridi lenye fumbo …………..                             Utuombee
Mnara wa Daudi …………..                                    Utuombee
Mnara wa pembe …………..                                  Utuombee
Nyumba ya dhahabu …………..                           Utuombee
Sanduku la Agano …………..                 Utuombee
Mlango wa Mbingu …………..                               Utuombee
Nyota ya asubuhi …………..                                  Utuombee
Afya ya wagonjwa …………..                                Utuombee
Kimbilio la wakosefu …………..                          Utuombee
Mfariji wa wenye uchungu …………..               Utuombee
Msaada wa waKristo …………..                           Utuombee
Malkia wa Malaika …………..                                Utuombee
Malkia wa Mababu …………..                               Utuombee
Malkia wa Mitume …………..                                Utuombee
Malkia wa Mashahidi …………..                           Utuombee
Malkia wa Waungama  …………..                       Utuombee
Malkia wa Mabikira …………..                             Utuombee
Malkia wa Watakatifu wote …………..             Utuombee
Malkia uliyeumbwa pasipo dhambi ya asil.Utuombee
Malkia uliyepalizwa Mbinguni…………           Utuombee
Malkia wa Rozari takatifu …………..                 Utuombee
Malkia wa amani …………..                                   Utuombee

Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusamehe ee Bwana.

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusikilize ee Bwana

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utuhurumie.

SALA YA KUMUOMBA
MT. THERESIA WA MTOTO YESU

Ee Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu, ulistahili kuitwa Msimamizi wa Misioni Katoliki za Dunia yote.  Kumbuka ile tama yako kuu uliyoonyesha huku Duniani ya “kusimika Msalaba wa Yesu Kristo, katika Nchi zote na kuhubiri Injili mpaka mwisho wa dunia”  twaomba kwa ajili ya maagano yako, wasaidie Mapadre, Wamisionari, na Kanisa zima.   Ee Mtakatifu  Theresia wa Mtoto Yesu Msimamizi wa Misioni:  Utuombee


Tuombe:  Ee Mtakatifu Theresia mdogo wa Mtoto Yesu, nakuomba unichumie waridi kutoka kwenye bustani ya Mbinguni na unitumie kama ujumbe wa upendo. Ewe waridi dogo la Yesu, umwombe Mungu anijalie neema hii ninayoiweka mikononi mwako...
(taja ombi lako) 

      Mt. Teresia, kama wewe,unisaidie mimi pia niuamini upendo wa Mungu kwangu,ili kila siku niingie "Njia yako ndogo".  AMINA.

SALA  YA  JUBLEI YA MIAKA  150  YA  UKRISTO,
TANZANIA  BARA
Ee  Mungu Mwenyezi/Baba wa milele/tunakushukuru kwa sababu ya Mwanao Mpendwa Yesu Kristo/aliyetwaa Mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu/akazaliwa na Bikira Maria. /Yeye alihubiri neno lako/ na kukamilisha ukombozi kwa mateso/kifo na ufufuko wake wa ajabu. /Hatimae aliwaagiza Mitume wake akisema/ “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe./ Aaminiye na kubatizwa ataokoka/asiye amini atahukumiwa  (Mk  16:15-16).

Kwa kuitika agizo hilo/ wakati ulipowadia/ kwa mapenzi yako uliwavuvia  Watawa mashuhuri wa Shirika la Roho Mtakatifu/ ambao kwa ujasiri  wa ajabu walifika  huku kwetu/ wakausimika Msalaba katika kituo cha Bagamoyo./  Msalaba huo ni Ishara ya ushindi wa Mwanao dhidi ya dhambi na mauti ./  Wamisionari hao wakishirikiana na wenzao waliofika baadaye/ walikuhubiri wewe./  Nasi tuliopata Imani kwa Mahubiri yao/ tunakukiri wewe kuwa Bwana Mungu wetu/ mwingi wa Huruma/ Mwenye Fadhila/ si mwepesi wa hasira/ mwingi wa Rehema na kweli/ (Ayubu  4:3).
Basi, tunaposherekea JUbilei ya Miaka 150 ya Kanisa Katoliki Tanzania Bara/ Tunakuabudu katika Maongozi yako./  Tunakushukuru kwa kuongezeka kwa Imani/  inayoonekana katika Idadi ya Waamini Walei/ Makatekista/ Watawa Mapadri na Maaskofu wazalendo./  Tunakushukuru kwa kutuwezesha kuhudumia Taifa letu katika Elimu/ Afya na huduma nyingine  za jamii.

Tunajua kuwa bila wewe hatuwezi kitu/  tunakuomba uwe pamoja nasi katika kukimbiliana na changamoto mbalimbali kwenye Taifa letu siku hizi hasa/  Ulevi wa Pombe na dawa za kulevya/  usafirishaji haramu wa Binadamu/ Ugaidi/  Maradhi/  Ubakaji/  Ulawiti/  Ushirikina na Ulegevu wa Dini.

Tunamwomba Mama Bikira Maria/  Nyota ya Uinjilishaji mpya/  na Mlinzi wa Taifa  letu/  atuombee kwako daima /  ili tuendelee kuihubiri  Injili yako katika Maisha yetu ya kila siku.

Tunaomba hayo kwa Njia ya Kristo Bwana wetu.  Amina
Sala hii imetayarishwa na Mhashamu Askofu
Tarcisius Ngalalekumtwa
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki-Tanzani