KIONGOZI NI NANI
Sehemu Ya Kwanza
Watu wanaweza kuwa viongozi kutokana na sifa au karama aliyojaliwa na
Mungu. Kiongozi naweza akawa mtu aliyesomea pia kuna baadhi ya watu wao
huzaliwa wakiwa na karama hiyo ya
uongozi, watu hawa wanaweza wakawa viongozi wazuri sana pengine kupita hata
wale waliosomea.
Katika ulimwengu watu kuna aina mbili za viongozi;-
1.
Viongozi
wa kuchaguliwa
2.
Viongozi
wa kuteuliwa/kurithi
****************
MAJUKUMU YA
KIONGOZI;-
i.
Kutekeleza
majukumu aliyopewa na watu
iii.
Kusimamia
raslimali za watu
iv.
Kusimamia
na kulinda “ukweli” katika kuleta
maendeleo ya watu
Kiongozi akitimiza majukumu hayo atakuwa ni
kiongozi mzuri na mwenye kupendwa na watu kwa sababu ya utumishi wake mzuri kwa watu. Watu wanaweza
kutamani na kuonja maisha ya furaha kupitia yeye, na ndivyo ilivyo kwa kiongozi
mzuri anayejali na kutekeleza majukumu yake.
UONGOZI MBAYA;-
Katika uongozi kuna baadhi ya watu wao hutumia Mamla hayo ya uongozi
kufanya ndivyo sivyo kwa sababu ya manufaa yao binafsi. Jambo hili huathili
sana watu wanyonge wanaotegemea viongozi wao kufaya kadri ya matakwa na misingi
ile uliyompelekea yeye kuchaguliwa au kuteuliwa na watu. Kiongozi anaweza akawa kikwazo kwa watu kwa
sababu ya kutumia nguvu na mamlaka aliyopewa kunyanyasa watu na kuhujumu mali
na haki ya binadamu.
Asilimia
kubwa ya watu wanaotarajia kuteuliwa au kuchaguliwa huwa ni wazuri wa kushawishi
na huwa wanamvuto flani kabla hawajawa viongozi, hawa hufanya hivyo kwa sababu
bado hawajapata uongozi, na huwa ni watu wa watu sana.
Uongozi
vile vile unaweza kumtia mtu ‘ujinga’ au ‘ukatili’ kwa sababu ya mitazamo binafsi. Uongozi unawafanya viongozi wa Serikali pia Dini,
kutumia uongozi huo waliopewa kunyanyasa watu.
Wao hujiona ni bora sana kupita watu wengine, wao hujiona si wakosefu,
wao hujiona wapo sawa katika kile wanachokifanya, wao huyaona makosa ya watu
wengine kuliko yao, wao hulimbikiza makosa yao kwa vijakazi wao waonekane
wazuri, wao huwaona ni watumwa na watu wasiojielewa watumishi wengine. Hizi ni
baadhi ya sifa za viongozi wanaotumia mamlaka yao vibaya.
********************************
Inaendelea……………………………..
Mayumba Publisher
Msalala-Kahama, Contact.
+2257-6925-3139
Author; John Christopher

No comments:
Post a Comment