ROZARI YA
HURUMA YA MUNGU
HISTORIA YA
TOKEO LA HURUMA
DUNIANI
Sista Faustina alizaliwa tarehe 25 August 1905 katika kijiji cha Glogowieko nchini Poland, na jina lake la ubatizo lilikuwa Helena.
Akiwa na umri wa Miaka 20, Bwana alimwongoza kuingia katika utawa wa shirika la Mama wa Huruma ambako (kama kawaida) alibadilisha jina na kuitwa Sista Maria Faustina, akaweka nadhiri za kwanza mwaka 1928.
Sista Faustina alizaliwa tarehe 25 August 1905 katika kijiji cha Glogowieko nchini Poland, na jina lake la ubatizo lilikuwa Helena.
Akiwa na umri wa Miaka 20, Bwana alimwongoza kuingia katika utawa wa shirika la Mama wa Huruma ambako (kama kawaida) alibadilisha jina na kuitwa Sista Maria Faustina, akaweka nadhiri za kwanza mwaka 1928.
MATUKIO
Bwana Yesu alianza kumtokea Sista Faustina mfululizo tangu mwaka 1930 hadi 1938. Alimtokea ili kumwandaa kwa ujumbe mkubwa wa maisha wa kuiangazia dunia nzima Ibada ya Huruma ya Mungu, ambayo ilikuwa na madhumuni yafuatayo;
Bwana Yesu alianza kumtokea Sista Faustina mfululizo tangu mwaka 1930 hadi 1938. Alimtokea ili kumwandaa kwa ujumbe mkubwa wa maisha wa kuiangazia dunia nzima Ibada ya Huruma ya Mungu, ambayo ilikuwa na madhumuni yafuatayo;
- Kuandaa ujio wa Pili wa Bwana wetu
Yesu Kristo aliye Mfalme wa Huruma.
- Kuokoa roho zilizoko Toharani.
- Kuwaongoa wakosefu ambao
wameshapoteza neema ya kujiombea.
- Kuitangaza Huruma ya Mungu.
Tarehe 22 Februari 1931 alipokuwa na umri wa miaka 26, Sista Faustina
alitokewa kwa mara ya kwanza na Bwana Yesu na kumchagua kuwa mjumbe wa Ibada ya
Huruma ya Mungu. Sista Faustina anatueleza:
"Mchoro halisi wa Huruma Kuu,
uliochorwa
chini ya usimamizi wa Sista
Faustina"
mwanga
inayong'ara. Miale ya upande wa kulia ilikuwa myekundu na miale ya upande wa
kushoto ilikua myeupe"
Sista Faustina hakujua maana ya aina hizo mbili za
miale ya mwanga aliyoiona, na siku moja alimuuliza Bwana Yesu maana yake. Bwana
Yesu kwa utulivu mkubwa alimwambia, "Miale miwili hiyo ya mwanga inayotoka ndani ya moyo wangu ni alama ya
Damu na Maji yaliyomwagika kutoka katika Moyo wangu wenye Huruma, siku ile
nilipojitoa sadaka Kalvarini.
Miale Myeupe ni alama ya Maji
yanayoosha roho na miale Myekundu ni alama ya Damu inayoleta uzima wa Roho za
watu. Miale hii inalinda Roho kabla ya adhabu ya Baba yangu: Kwa anayeishi
katika ulinzi wake (Miale hiyo), mkono wa Hasira ya Mungu hautamfikia kamwe’’.
Kisha Bwana Yesu alimfundisha Sista
Faustina sala hii: "Ee Damu na Maji
vinavyotoka katika Moyo Mtakatifu wa Yesu, kama chanzo cha Huruma yake,
ninakutumaini"
Bwana Yesu huku akimwonyesha Moyo wake Mtakatifu alimwambia Sista Faustina "Chora picha kama unavyoona, na uandike YESU NINAKUTUMAINIA. Mimi ni Mfalme wa Huruma.
“Ninatamani picha hii iwekwe na kuheshimiwa kwanza Kanisani kwako na baadaye Ulimwenguni kote. Naahidi ushindi kwake na maadui zake walio Duniani na hasa saa ya kufa kwake. Mimi mwenyewe nitamlinda. Kwa njia ya picha hii nitatoa neema nyingi kwa watu watakaoitunza vizuri, hata kwa wale watakaoitazama"
Bwana Yesu huku akimwonyesha Moyo wake Mtakatifu alimwambia Sista Faustina "Chora picha kama unavyoona, na uandike YESU NINAKUTUMAINIA. Mimi ni Mfalme wa Huruma.
“Ninatamani picha hii iwekwe na kuheshimiwa kwanza Kanisani kwako na baadaye Ulimwenguni kote. Naahidi ushindi kwake na maadui zake walio Duniani na hasa saa ya kufa kwake. Mimi mwenyewe nitamlinda. Kwa njia ya picha hii nitatoa neema nyingi kwa watu watakaoitunza vizuri, hata kwa wale watakaoitazama"
2. Baba Yetu
3. Salamu Maria
4. Kanuni ya
Imani
Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi, Muumba
mbingu na Dunia na kwa Yesu Kristo, Mwanaye wa pekee Bwana wetu, aliyetungwa
kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya
Ponsyo Pilato, akasulibiwa, akafa, akazikwa
akashukia kuzimu siku ya tatu akafufuka kadiri ya maandiko, akapaa mbinguni
ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi toka huko atakuja kuwahukumu wazima na
wafu, Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa Takatifu Katoliki, Ushirika wa
Watakatifu, maondoleo ya dhambi , Ufufuko wa Miili na Uzima wa Milele. Amina
5. Baba wa Milele, ninakutolea
Mwili na Damu, Roho na Umungu wa Mwanao Mpenzi sana, Bwana wetu Yesu Kristo,
Kwa malipizi ya dhambi zetu na za Dunia nzima.
6. K. Kwa ajili ya mateso makali ya
Bwana
wetu Yesu Kristo.
W. Utuhurumie sisi na Dunia nzima
7. MWISHO
K. Ewe Damu na
Maji aliyemwagika kutoka Moyoni
mwa Yesu kama Chemuchemu ya
Huruma kwetu.
W. Tunakutumainia
K . Mungu Mtakatifu,
Mtakatifu Mwenye Enzi,
Mtakatifu unayeishi
milele x 3
LITANIA YA HURUMA YA MUNGU
Bwana utuhurumie – - - Bwana
utuhurumie
Kristu utuhurumie – - - Kristu utuhurumie
Kristu utuhurumie – - - Kristu utuhurumie
Bwana
utuhurumie – - - Bwana
utuhurumie
Kristu utusikie – - - Kristu utusikilize
Baba wa mbinguni Mungu – - - utuhurumie
Mwana Mkombozi wa dunia Mungu - - utuhurumie
Roho Mtakatifu Mungu - - - utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu mmoja utuhurumie.
Kristu utusikie – - - Kristu utusikilize
Baba wa mbinguni Mungu – - - utuhurumie
Mwana Mkombozi wa dunia Mungu - - utuhurumie
Roho Mtakatifu Mungu - - - utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu mmoja utuhurumie.
Huruma
ya Mungu iliyo sifa kuu ya Muumba wetu - - -
Tunakutumaina
Huruma
ya Mungu iliyo kilele cha ukamilifu wa Mwokozi wetu
Tunakutumaina
Huruma
ya Mungu iliyo upendo usiopimika wa Roho Mtakasa
Tunakutumaina
Huruma
ya Mungu fumbo lisilofahamika la Utatu Mtakatifu
Tunakutumaina
Huruma
ya Mungu iliyo ishara ya uwezo mkuu wa Mungu Mwenyezi Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu iliyofumbuliwa katika kuziumba Roho za Malaika wa mbinguni Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu iliyotuumba na kutuamuru tuwepo bila kutokana na chochote Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu inayotujalia maisha ya kutokufa
Tunakutumaina
Huruma
ya Mungu inayotukinga na adhabu tunazostahili
Tunakutumaina
Huruma
ya Mungu inayotuinua tutoke katika taabu, unyonge na maumivu ya dhambi zetu Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu inayotufanya wenye haki katika Neno aliyejifanya Mtu Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu iliyotupatia Bikira Maria Mtukufu awe kwetu Mama wa Huruma Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu iliyoonyeshwa katika kuanzishwa Kanisa Katoliki Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu inayotolewa kwa wanadamu wote kwa njia ya Sakramenti ya Ubatizo na
Kitubio Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu inayotolewa katika Sakramenti ya Ekaristi na Upadrisho Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu inayoonyeshwa kwetu pale inapotuita na kutuingiza katika
kuwatakatifuza wenye hakiTunakutumainia
Huruma
ya Mungu inayotimilika katika ukamilifu wa watu watakatifu Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu chemchemi ya afya kwa wagonjwa na wote wanaoteseka Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu iliyo faraja ya wote wenye uchungu moyoni
Tunakutumaina
Huruma
ya Mungu iliyo tumaini la roho zinazosumbuliwa na mkato wa tama Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu iliyo mwenzi wa daima na popote wa watu wote Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu inayowahi kutuletea neema zake
Tunakutumaina
Huruma
ya Mungu iliyo amani yao wanaokufa
Tunakutumaina
Huruma
ya Mungu iliyo burudisho na faraja yao marehemu wa toharani Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu iliyo furaha ya mbinguni kwa watakatifu wote
Tunakutumainia
Huruma
ya Mungu iliyo taji la watakatifu wote
Tunakutumaina
Huruma
ya Mungu chemchemi ya miujiza isiyokauka
Tunakutumaina
Huruma ya Mungu inayofurika kutoka
katika majeraha ya Kristu Tunakutumaina
Huruma
ya Mungu inayobubujika kutoka ndani ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Tunakutumaina
Mwanakondoo
wa Mungu uliyetuonyesha huruma yako kuu
katika
kuikomboa dunia kwa msalaba wako mtakatifu, -
utusamehe ee Bwana
Mwanakondoo
wa Mungu unayejitolea kwetu kwa mapendo na
huruma
katika kila adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu,-
utusikilize
ee Bwana
Mwanakondoo
wa Mungu anayeondoa dhambi za dunia kwa njia ya huruma yako isiyo na mwisho,- utuhurumie.
K. Bwana
utuhurumie –
W. Bwana
utuhurumie.
K. Kristo utuhurumie, -
K. Kristo utuhurumie, -
W. Kristo utuhurumie
K. Huruma anana za Bwana zi juu ya kazi zake
K. Huruma anana za Bwana zi juu ya kazi zake
zote –
W. Huruma
za Bwana nitaziimba milele.
TUOMBE:
Ee Mungu uliye na huruma isiyo na mwisho, na hazina za wema na upendo
wako hazina mipaka. Tunakusihi ututazame sisi watu wako huku duniani na
kutuongezea huruma yako tena na tena, ili itusaidie tusije tukakata tamaa hata
mara moja, haidhuru tukumbane na majaribu makubwa kiasi gani, bali tuweze daima
kuzielekea na kuzishika amri zako, kwa matumaini na kutimiza mapenzi yako
matakatifu, ambayo ndiyo huruma yenyewe. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu
Yesu Kristu Mwanao, Mfalme wa Amani na Huruma, aishiye na kutawala nawe, na
Roho Mtakatifu, kwa pamoja mkituonyesha huruma, daima na milele. Amina.
ROZARI
TAKATIFU YA BIKIRA MARIA
HISTORI FUPI YA ROZAR
YA BIKIRA MARIA
Neno Rozari limetokana na neno la
Kilatini "Rosarium" lenye maana ya Taji la
Mawaridi. Neno “WARIDI” katika maana
halisi na sahihi ni ni moja kati ya Ua lenye muonekano Mzuri na lenye kuvutia
sana kwa maana fupi Waridi ni “Alama ya
Ushindi” na sisi Mama Maria anatuhimiza tumweze kumpa “Waridi” kila
tusalipo Rozari kwa kuwa katika Rozari ndiko Upendo wake kwetu ulimo. Mama yetu
Bikira Maria aliwafahamisha baadhi ya watu aliowatokea kuwa kila mara mtu
anaposali sala ya "Salamu
Maria" anampa mama Maria waridi na hivyo kila anayesali rozari
nzima humkabidhi mama Maria taji la mawaridi. Rozari imegawanyika katika
matendo yafuatayo: Matendo ya FURAHA, UCHUNGU na UTUKUFU. Na mnamo October 16, 2002 Baba Mtakatifu
marehemu John Paul II aliongeza matendo mengine ambayo yaliitwa matendo ya MWANGA. Rozari Takatifu hujulikana
kama sala kamili kwa sababu ndani yake hupatikana Historia kamili ya ukombozi
wetu sisi wanadamu. Katika Rozari tunatafakari matendo ya Furaha, Uchungu
na Utukufu ambayo yanaelezea historia nzima ya maisha
ya Bwana wetu YESU KRISTO na ukombozi uliopatikana katika yeye
kwetu sisi wanadamu kupitia Msalaba.
Katika sala ya Salamu Maria tunamkaribisha Mama Maria atuombee sisi wanadamu kwa mwanawe Bwana wetu YESU KRISTO hivyo kufanya sala zetu kuwa na nguvu zaidi mbele zake MUNGU.
Dhumuni kuu la kusali rozari ni kwa
ajili ya kuwaombea wakosefu waongoke na kumrudia MUNGU katika KRISTO YESU
mwanawe wa pekee aliyetukomboa dhidi ya yule muovu kwa mateso, kifo na ufufuko
wake. Kila mara mtu au watu wanapopiga magoti na kusali rozari mama Bikira
Maria huja haraka na kukaa pembeni yake/yao wanaosali na kusali nao,
NAMNA YA
KUSALI ROZARI YA BIKIRA
MARIA
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Kwa Jina la Baba na la Mwana na
la Roho Mtakatifu. Amina
(Tunasali Rozari Takatifu kwa Nia ya
/………………../)
1. KANUNI YA
IMANI (kwenye Msalaba)
Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi,
Muumba mbingu na Dunia na kwa Yesu Kristo, Mwanaye wa pekee Bwana wetu,
aliyetungwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa
kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato,
akasulibiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu siku ya tatu akafufuka kadiri ya
maandiko,akapaa mbinguni ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi toka huko
atakuja kuwahukumu wazima na wafu, Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa Takatifu
Katoliki, Ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi , Ufufuko wa Miili na
Uzima wa Milele. Amina
2. Baba Yetu (Punje Kubwa)
3. Salamu
Maria x 3 (Punje ndogo)
4. Atukuzwe Baba……. (Kwenye punje Kubwa)
K. Tuwasifu
Milele
W.
Yesu Maria na Yoseph
K. Ee
Yesu Mwema
W.
Utusamehe dhambi zetu utukunge na moto
wa Milele
ongoza Roho zote Mbinguni, hasa za wale
wanaohitaji
huruma yako
Taja
fumbo kisha (Baba Yetu)
5. Salamu
Maria x 10
6. Atukuzwe Baba……. (Kwenye
punje Kubwa)
K. Tuwasifu
Milele
W.
Yesu Maria na Yoseph
K. Ee
Yesu Mwema
W.
Utusamehe dhambi zetu utukunge na moto
wa Milele
ongoza Roho zote Mbinguni, hasa za wale
wanaohitaji
huruma yako
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea
Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe
Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili
yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)
Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwendambinguni.
Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
Tendo la tano; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
MATENDO YA MWANGA
(Alhamisi)
TENDO LA KWANZA; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe
Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
TENDO LA PILI; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
TENDO LA TATU; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
TENDO LA NNE; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
TENDO LA TANO; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
TENDO LA PILI; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
TENDO LA TATU; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
TENDO LA NNE; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
TENDO LA TANO; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
SALAMU MALKIA
Mama mwenye huruma, uzima, tulizo na
matumaini yetu, salamu, tuankusihi ugenini hapa sisi wana wa Eva. Tunakulilia,
tunalalamika na kuhuzunika bondeni huku kwenye machozi. Haya basi mwombezi wetuutuangalie kwa macho
yako yenye huruma. Mwisho wa ugeni huu, utuonyeshe Yesu mzao wa tumbo
lako. Ee mpole, Ee mwema, Ee mpendelevu,
Bikira Maria.
W. Utujalie
ahadi ya Kristo
Tuombe: Ee
Mungu, makimbilio na nguvu yetu, uwaangalie kwa wema watu wanao kulilia;
na kwa maombezi ya Bikira Maria Mtukufu asiye na kosa Mzazi wa Mungu, na ya
Mtakatifu Yosefu, mchumba wake, na ya Watakatifu wote: usikilize kwa huruma na
wema sala tunazokutolea kwa wongofu wa wakosefu na kwa
KUMBUKA
Kumbuka Ee Bikira mpole sana, haijasikilika kamwe kwamba ulimwacha mtu
aliyekimbilia ulinzi wako, aliyeomba msaada na maombezi yako.
Kwa matumaini hayo, nakukimbilia, Ee Mama, mkuu wa mabikira. Ninakuja kwako, nasimama mbele yako,
nikilalamika mimi mkosefu , Ewe Mama wa Neno wa Mungu. Naomba usikatae maneno yangu, bali uyasikilize. Amina
(Tunakimbilia Ulinzi wako……………………………….)
LITANIA YA BIKIRA MARIA
Bwana
utuhurumie Bwana
utuhurumie
Kristo utuhurumie Kristo
utuhurumie
Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie
Kristo utusikie Kristo utusikilize
Baba wa Mbinguni Mungu,…… Utuhurumie
Mwana Mkombozi wa dunia Mungu……… Utuhurumie
Roho Mtakatifu Mungu…….. Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja …….. Utuhurumie
Maria Mtakatifu ………. Utuombee
Mzazi Mtakatifu wa Mungu …….. Utuombee
Bikira Mtakatifu Mkuu wa Mabikira …….. Utuombee
Mama wa Neema ya Mungu ………….. Utuombee
Mama Mtakatifu sana ……… Utuombee
Mama mwenye usafi wa Moyo ……….. Utuombee
Mama usiye na doa ……….. Utuombee
Mama usiye na dhambi…… Utuombee
Mama mpendelevu ………. Utuombee
Mama mstajabivu ………. Utuombee
Mama wa shauri jema Utuombee
Mama wa Muumba ………. Utuombee
Mama wa Mkombozi ………….. Utuombee
Bikira mwenye utaratibu ………….. Utuombee
Bikira mwenye heshima ………….. Utuombee
Bikira mwenye sifa ………….. Utuombee
Bikira mwenye enzi ………….. Utuombee
Bikra mweye huruma ………….. Utuombee
Bikra amini………….. Utuombee
Kioo cha haki ………….. Utuombee
Kikao cha hekima ………….. Utuombee
Sababu ya furaha yetu ………….. Utuombee
Chombo cha neema ………….. Utuombee
Chombo cha heshimiwa ………….. Utuombee
Chombo bora cha Ibada ………….. Utuombee
Waridi lenye fumbo ………….. Utuombee
Mnara wa Daudi ………….. Utuombee
Mnara wa pembe ………….. Utuombee
Nyumba ya dhahabu ………….. Utuombee
Sanduku la Agano ………….. Utuombee
Mlango wa Mbingu ………….. Utuombee
Nyota ya asubuhi ………….. Utuombee
Afya ya wagonjwa ………….. Utuombee
Kimbilio la wakosefu ………….. Utuombee
Mfariji wa wenye uchungu ………….. Utuombee
Msaada wa waKristo ………….. Utuombee
Malkia wa Malaika ………….. Utuombee
Malkia wa Mitume ………….. Utuombee
Malkia wa Mashahidi ………….. Utuombee
Malkia wa Waungama ………….. Utuombee
Malkia wa Mabikira ………….. Utuombee
Malkia wa Watakatifu wote ………….. Utuombee
Malkia uliyeumbwa pasipo dhambi ya asil.Utuombee
Malkia uliyepalizwa Mbinguni………… Utuombee
Malkia wa Rozari takatifu ………….. Utuombee
Malkia wa amani ………….. Utuombee
Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za
dunia,…………..Utusamehe ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za
dunia,…………..Utusikilize ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za
dunia,…………..Utuhurumie.
SALA YA KUMUOMBA
MT. THERESIA WA MTOTO YESU
Tuombe: Ee Mtakatifu Theresia mdogo wa Mtoto Yesu, nakuomba unichumie waridi kutoka kwenye bustani ya Mbinguni na unitumie kama ujumbe wa upendo. Ewe waridi dogo la Yesu, umwombe Mungu anijalie neema hii ninayoiweka mikononi mwako...
(taja ombi
lako)
Mt. Teresia, kama wewe,unisaidie mimi pia niuamini upendo wa Mungu kwangu,ili kila siku niingie "Njia yako ndogo". AMINA.
SALA
YA JUBLEI YA MIAKA 150
YA UKRISTO,
TANZANIA
BARA
Ee
Mungu Mwenyezi/Baba wa milele/tunakushukuru kwa sababu ya Mwanao Mpendwa
Yesu Kristo/aliyetwaa Mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu/akazaliwa na Bikira
Maria. /Yeye alihubiri neno lako/ na kukamilisha ukombozi kwa mateso/kifo na
ufufuko wake wa ajabu. /Hatimae aliwaagiza Mitume wake akisema/ “Enendeni
ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe./ Aaminiye na kubatizwa
ataokoka/asiye amini atahukumiwa
(Mk 16:15-16).
Kwa kuitika agizo hilo/ wakati ulipowadia/
kwa mapenzi yako uliwavuvia Watawa
mashuhuri wa Shirika la Roho Mtakatifu/ ambao kwa ujasiri wa ajabu walifika huku kwetu/ wakausimika Msalaba katika kituo
cha Bagamoyo./ Msalaba huo ni Ishara ya
ushindi wa Mwanao dhidi ya dhambi na mauti ./
Wamisionari hao wakishirikiana na wenzao waliofika baadaye/ walikuhubiri
wewe./ Nasi tuliopata Imani kwa Mahubiri
yao/ tunakukiri wewe kuwa Bwana Mungu wetu/ mwingi wa Huruma/ Mwenye Fadhila/
si mwepesi wa hasira/ mwingi wa Rehema na kweli/ (Ayubu 4:3).
Basi, tunaposherekea JUbilei ya Miaka 150 ya
Kanisa Katoliki Tanzania Bara/ Tunakuabudu katika Maongozi yako./ Tunakushukuru kwa kuongezeka kwa Imani/ inayoonekana katika Idadi ya Waamini Walei/
Makatekista/ Watawa Mapadri na Maaskofu wazalendo./ Tunakushukuru kwa kutuwezesha kuhudumia Taifa
letu katika Elimu/ Afya na huduma nyingine
za jamii.
Tunajua kuwa bila wewe hatuwezi kitu/ tunakuomba uwe pamoja nasi katika
kukimbiliana na changamoto mbalimbali kwenye Taifa letu siku hizi hasa/ Ulevi wa Pombe na dawa za kulevya/ usafirishaji haramu wa Binadamu/ Ugaidi/ Maradhi/
Ubakaji/ Ulawiti/ Ushirikina na Ulegevu wa Dini.
Tunamwomba Mama Bikira Maria/ Nyota ya Uinjilishaji mpya/ na Mlinzi wa Taifa letu/
atuombee kwako daima / ili
tuendelee kuihubiri Injili yako katika
Maisha yetu ya kila siku.
Tunaomba hayo kwa Njia ya Kristo Bwana
wetu. Amina
Sala hii
imetayarishwa na Mhashamu Askofu
Tarcisius
Ngalalekumtwa
Rais wa Baraza
la Maaskofu Katoliki-Tanzani

No comments:
Post a Comment